Om Haile Ngoma ya Wana
Diwani hii imeandikwa kwa lahaja ya Kimvita, lahaja izungumzwayo jijini Mombasa. Lahaja hii imetumiwa na washairi maarufu pamoja na wazoefu wa tungo katika nyakati mbalimbali kihistoria kama vile Shaha Muyaka wa Muhaji, Ahmad Nassir Juma Bhalo, Abdilatif Abdalla na sasa Ahmed Hussein Ahmed. Hii ni lahaja yenye manyumbulifu anuwai kwa namna sauti zake zinavyoleta maana tafauti zinapotamkwa na ina ukwasi wa misamiati. Mashairi yaliyomo kwenye diwani hii yanaangazia mada mbalimbali zikiwemo, utamaduni wa mwandishi, masuala ya maisha, mijadala ya kielimu, maswali na majibu, taanasi and masuala ya kisasa. Vile vile mshairi ametumia mbinu mbalimbali za tasnifu ya tungo kwa mfano, tathlitha, tarbia na majibizano kufikisha ujumbe wake.
Visa mer