Om Upendo
Neno 'Sheria' linatokana na neno la Kiebrania 'Torah', ambalo maana yake ni 'maagizo', na 'somo'. Torah kwa kawaida linarejelea Pentatuki (vitabu vitano vya Biblia) vinavyojumuisha Amri Kumi. Lakini, "Sheria" pia linerejelea vitabu 66 vya Biblia kwa jumla, au yale maagizo ya Mungu anapotuambia cha kufanya, cha kutofanya, cha kuweka, au kutupilia mbali mambo fulani. Huenda watu wakafikiria kwamba Sheria na upendo havihusiani, lakini haviwezi kutenganishwa. Upendo ni wa Mungu, na pasipo kumpenda Mungu hatuwezi kuifuata Sheria kikamilifu. Sheria inaweza kutimizwa tu tunapoifuata kwa upendo.
Visa mer