Om Nukuu za Nyakati Zetu
Kitabu cha Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu ni mkusanyiko wa nukuu za Enock Maregesi, kila nukuu kuu na maana yake, kila siku na nukuu yake kwa mwaka mzima. Ni mkusanyiko wa nukuu kuu 365 zenye kuleta hamasa na msukumo wa mafanikio katika maisha ya mtu.
Lengo la kitabu hiki ni mtu kuwa na nukuu katika kila jambo katika kila hali katika kila kipengele cha maisha yake, kupata amani ya moyo na uhuru wa nafsi, kama msingi wa mafanikio, katika maendeleo ya maisha yake kwa ujumla wake.
Ukitaka kujitambua katika maisha yako jijibu maswali yafuatayo: Wewe ni nani? Umetoka wapi? Kusudi la maisha yako ni nini hapa duniani? Kisha tengeneza dira ya maisha ya nyuzi 360 inayozidi hata hatima ya maisha yako ya hapa.
Kitabu cha Falsafa za Enock Maregesi: Nukuu za Nyakati Zetu kitakusaidia kutengeneza dira ya maisha inayozidi maisha yako ya hapa duniani. Aidha, kitakusaidia kupata angalau nukuu 12 za kwako mwenyewe zitakazokuongoza na kukupeleka katika mafanikio yako ya kimwili na ya kiroho pia.
Visa mer